Kalapina Afunguka Kuhusu Chid Benz Kurudia Madawa
Msanii Kalapina ambaye pia ni mwanaharakati wa kupambana na madawa ya kulevya na akiwa mmoja wa watu waliomsaidia Chid Benz baada ya kuathiriwa na madawa ya kulevya, amefunguka kuhusu hali ya sasa ya msanii huyo.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Kalapina amesema Chid Benz alikuwa hajapata matibabu sahihi alipotoka ‘sober house’, hivyo amemtaka kurudi na kuwasikiliza watu waliomsaidia ili asifikie pabaya.
“Chid Benz hakumaliza muda wa matibabu alivyotoka ‘sober house’ ndani ya siku 28, kwahiyo mi namuomba afikirie faida alizozipata sober na faida anazozipata sasa hivi akiwa mtaani, nafasi bado ipo kwake kwa sababu tumeplay part kubwa hadi Chid Benz akae sawa, kwa hiyo anatakiwa atusikilize, nafasi ipo kubwa kwa Chid Benz kuweza kujisahihisha”, alisema Kalapina.
Kalapina aliendelea kutufungulia na yale ambayo yalikuwa hayajifika kwenye vyombo vya habari kuwa msanii huyo (Chid Benz) na msanii Ray C ambaye pia ni muathirika na madawa ya kulevya, walipata wafadhili wa kuwapeleka nchi za nje kwa matibabu zaidi, lakini ikashindikana kutokana na kitendo hicho.
“Kulikuwa kuna safari ya yeye na Ray C kupelekwa Ulaya, wafadhili walikuwa wanataka kuwapeleka Ulaya kwa matibabu zaidi, lakini ilitakiwa subira kidogo, ndani ya siku 28 yeye amechoka kukaa sober anataka kukaa mtaani, sasa wafadhili wakishaona uko mtaani tena ku’invest hela yao inakuwa ngumu wanaona bado hujapona”, alisema Kalapina.
Pia Kalapina amekanusha suala la kwamba walimtelekeza msanii huyo, kwani walikuwa wanakwenda kumtembelea na kumpelekea mahitaji yote muhimu.
eatv.tv