Eshe Buhet: Katu Sitamuonesha Mume Wangu
Mengi yamekuwa yakiongelewa kuhusu nyota huyu wa filamu za Kibongo, Eshe Buhet, huku ikiwepo minong’ono kuwa ndoa yake imevunjika.
Akizungumzia hilo anasema bado yupo kwenye ndoa na anaishi kwa amani na mume wake ingawa watu wanasambaza maneno kuwa wametengana.
“Niliolewa tangu mwaka 2008, nimefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike na ninaishi kwa amani na upendo na mume wangu. Nashangaa ambao wanasema nimeachika, mimi nipo katika ndoa yangu na sitarajii kuachika kwani najua kuchukua majukumu yangu kama mama.
“Nawajua Wabongo, wameanzisha maneno hayo ili nimuonyeshe mume wangu kwenye mitandao, katu sitafanya hivyo. Sifanyi maisha kwa ajili ya watu, naishi maisha yangu halisi.
“Wapo mastaa wenye tabia ya kuwaonyesha wapenzi au waume zao kwenye mitandao, ni wao. Siyo mimi na hatuwezi wote kufanana, kwangu halina nafasi,” anasema na kuongeza:
“Kuna mengi ya kufanya kwa ajili ya kuboresha ndoa, hayo ndiyo yana umuhimu kwangu, ndiyo maana nimeweza kudumu kwenye ndoa kwa miaka 13 mpaka sasa, si mchezo. Si jambo dogo. Namshukuru Mungu kwa ajili ya hilo.”
eatv.tv