-->

Exclusive Teaser: Filamu Mpya ya “The Foundation” ya J.Plus wa Misukosuko

Watakushangaa sana pale utakapo zungumzia Tasnia ya filamu za Action Tanzania bila kumtaja Mwasisi wa Filamu hizo Jimmy Mponda maarufu kama J.Plus ambaye ndiye miliki wa ‘Mzimuni Theatre Arts’ aliyewahi kushikiria ubora wake miaka 5 kwa filamu yake ya “Misukosuko” yaani 2005-2010.

jplus55
Kwa madai yake J.Plus, amesema kuwa baada ya kufanya vizuri kwa muda mrefu miaka kadhaa iliyopita, kisha kukaa kimya ili kuwaachia nafasi wasanii wengine waweze kuonesha uwezo wao katika Tasnia hio, kwa sasa amedai ni wakati wake tena.
Kwa maana hiyo J.Plus ameamua kurejea tena ulingoni ili kuitetea tasnia hiyo coz ameona kama ina legea legea na huenda ikapoteza ubora kwa mashabiki wa Filamu za Action Tanzania.
Baada ya siku chache, J.Plus anategemea kuachia Filamu yake mpya inayoitwa “The Foundation” ambayo ndani yake amecheza pia Inspector Seba. Akipiga stori na mwandishi J.Plus alimaliza kwa kusema,
“Kwanza Nashukuru Mungu kwa uzima, ukimya wangu haukuwa wa nia mbaya bali ni katika harakati za kuboresha kazi zangu, na kuangalia nini niwaletee mashabiki wangu ili walizike. Ujio huu utakuwa katika kasi kubwa maana lengo ni kutoa kitu juu ya kitu, Nitaanza na Filamu ya “The Foundation” ambayo nimecheza na Inspector Seba ‘I hope’ itarudisha heshima ya Action Movies Tanzania. Ombi langu kwa watanzania ni mapokezi mema kutoka kwao ushauri na maoni pia ni muhimu kwenye ufanisi wa kazi zetu asante”

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364