-->

Faida za Urasimishaji Tasnia ya Filamu 2015 Ina Msaada kwa Mdau?

Na Ignas Mkindi
Kabla mnaonishutumu inbox hamjanihukumu niwaeleze nnachoelewa mimi….
Kwa makadirio ya filamu 1329 zilizokaguliwa na kupewa madaraja:
1.Kwa wastani wa filamu moja kuwa na masaa mawili yaani part 1&2, Bodi ya Filamu imeingiza shilingi 159,480,000 kwa ukaguzi na kama walahu robo zilipewa vibali vya kushuti, bodi ilipata tena 165,000,000. Jumla ya shilingi 324,480,000 ziliingia Bodi ya Filamu.

Nape-Nnauye-532

Mh. Waziri akiwa katika moja ya maduka yanayouza kazi bandia Kariakoo.

2.Kwa makadirio hayo ya idadi, COSOTA watakuwa wameingiza 13,290,000 kwa kutoa clearance.
3.Kama kila filamu ilizalishwa walahu kopi 5000 ambacho ndiyo kima cha chini cha nakala ktk urasimishaji, TRA ilikusanya 112,965,000 kwa mauzo ya stempu. Na kama nusu ya filamu hizo ziliuzwa, TRA ilikusanya shilingi 146,190,000 kama revenue. Jumla TRA ilikusanya shilingi 259,155,000.
INA MAANA URASIMISHAJI ULIINGIZIA SERIKALI TSHS.596,925,000.
Upande wa wadau kwa makadirio hayo, kiasi chote hicho cha Tshs.596,925,000 zimetoka mifukoni kwao na nakala 3,322,500 zimedoda madukani zikiwa na thamani ya Tshs.2,990,250,000 (ikiwa nakala moja imedurufiwa kwa tshs.900). Jumla wadau wameunguza Tshs.3,587,175,000.

MATOKEO YAKE
1.Wasanii waliokuwa wanapewa mitaji na wasambazaji wamefutiwa mikataba, na sasa hawana sehemu ya kupata mitaji kwani taasisi za kifedha haziwezi kuwaamini kwani hawana thamana.
2.Makampuni yote makubwa yanayosambaza filamu yako ICU
3.Wasanii wengi walioanza kujikwamua kwa kusambaza kazi zao wenyewe sasa hivi wamehamia ktk tamthilia, mitaji imeyumba.
4.Uwekezaji umekuwa mdogo na kupelekea kuzalishwa filamu mbovu na kuzidi kuua soko la filamu za ndani.

5.Maduka karibia yote ya filamu mikoani yamebadili biashara.
LAKINI FAIDA MOJA KUBWA WALIYOPATA WASANII KWA MWAKA 2015, WALING’AA SANA KWENYE KAMPENI ZA UCHAGUZI WA RAIS NA WABUNGE NA ALHAMDULILLAH VIPOSHO WALIAMBULIA.
Nielekezeni mnachokijua ili nielimike ndio nicheze ngoma yenu.
1. MSANII ANANUFAIKA VIPI NA URASIMISHAJI?
2. URASIMISHAJI UMEINUA TASNIA NA WADAU WAKE KWA KIASI GANI?
Kama majibu hakuna hatujachelewa, tugeukie njia sahihi ambayo itajenga tija na kumaliza kile kilio kinacholiliwa kila siku kutoka kwa watu binafsi na Serikali ya kusema ajira kwa vijana maana filamu ndio alikuwa mkombozi wao.

Filamu Central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364