-->

Faiza: Sugu Akihitaji Mtoto, Namzalia!

MREMBO Faiza Ally ambaye aliwahi ‘kubanjuka’ penzini na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, ametoa kali ya aina yake kwa kusema, yupo tayari kumzalia mbunge huyo ambaye walishaachana miaka kibao iliyopita.
Kabla ya kumwagana na Sugu, mrembo huyo alifanikiwa kuzaa na mbunge huyo mtoto mmoja kisha kila mmoja akashika maisha yake.
Sugu kwa sasa ana maisha mengine na mchumba wake. Faiza naye alichukua hamsini zake na kufanikiwa kupata mtoto wa pili anayedai kuzalishwa na Raia wa Marekani.

Sugu, Faiza Ally na mtoto wao Sasha enzi za penzi lao

 

Pamoja jambo hilo, Faiza ambaye amekuwa hakaukiwi matukio kila uchwao, amefunguka mambo mengi kuhusiana na maisha yake kwa jumla;
Showbiz Extra: Ni changamoto gani umepata tangu umejifungua mtoto mwingine?

Faiza: Changamoto ilikuwa sijui ni jinsi gani ninaweza kugawa mapenzi kwa watoto wangu wawili, lakini Mungu ni mwema, nimeweza na sasa mimi na watoto wangu tunafurahi.
Showbiz Extra: Mtoto wa kwanza na huyu wa pili wote unawalea mwenyewe bila baba zao, ugumu gani unaupata?
Faiza: Sina ugumu wowote kwa sababu mtoto wangu huyu mwingine ameongeza furaha maradufu ndani ya nyumba na ‘usingo’ mama ninaukabili kabisa bila matatizo yoyote.
Showbiz Extra: Umekuwa katika kipindi cha misukosuko ya kumlea Sasha (mtoto wa Sugu), bila baba yake kwa muda mrefu sana, lakini umewezaje kuongeza mtoto mwingine ambaye utalea wewe peke yako pia?
Faiza: Unajua kila kitu kinatokea kwa sababu au mipango fulani. Huyu baba wa mtoto wangu wa pili ni Mmarekani na hatukupanga kuishi pamoja zaidi ya kuja mara moja kuona mtoto wake basi, hivyo tulivyoamua.

Showbiz Extra: Una mpango wa kuongeza mtoto mwingine?
Faiza: Hapana, tena hapa nikimaliza kunyonyesha nitaenda kufanya operesheni ya matiti kuyarudisha saa sita yaani nirudi msichana kabisa labda Sugu aseme anataka nimpe mtoto mwingine wa kiume nitafanya hivyo.
Showbiz Extra: Kwa hiyo akija na ombi hilo uko tayari, basi utakuwa bado unampenda?
Faiza: Ndiyo bado ninampenda kwani true love never die (penzi la kweli halifi).
Showbiz Extra: Watu wengi walikushangaa sana ulipoanza kuzurura na mtoto kabla ya siku 40, unazungumziaje hilo?
Faiza: Mimi kwangu 40 haina maana kabisa, ninachojua nimejifungua salama na ninashukuru maana vitu vingine ni watu wamejiwekea utaratibu wao wenyewe tu.
Showbiz Extra: Tayari sasa ni mama wa watoto wawili, vipi kuhusu yale mavazi yako utaacha?

Faiza: Siwezi kuacha wala kubadilika kwa sababu ni kitu ambacho ninacho hadi kwenye damu yangu.
Showbiz Extra: Ni kitu gani kiliwahi kukuumiza sana maishani?
Faiza: Niliumizwa tu kipindi kile mahakamani nilipotaka kunyang’- anywa mtoto kwa ajili ya mavazi yangu bila kuangalia ni jinsi gani ninalea mtoto.
Showbiz Extra: Una mpango gani miaka mitano ijayo?
Faiza: Nataka kuwa tajiri, nimiliki mjengo mkubwa, gari zuri na vitu vingi.
Showbiz Extra: Asante sana Faiza, nitakutafuta siku nyingine.
Faiza: Kuwa huru, karibu!
Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364