-->

Fella Kumuachia Mikoba Temba

Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanae Foundation pamoja na Yamoto Band, Mkubwa Fella amesema tayari ameshampata mtu sahihi ambaye atamwachia mikoba yake ya kusimamia wasanii pale atakapostaafu.

FELLA

Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii, Fella amesema amemuandaa msanii wa Kundi la TMK Family, Temba kuwa mrithi wake.

“Kusema kweli mtu ambaye nitamwachia kijiti ni Temba, tayari imeshamuandaa vya kutosha na bado naendelea, kwa hiyo Temba tayari anaelewa nini anatakiwa kufanya muda ukifika,” alisema Fella.

Kwa upande wa Temba amesema yupo tayari kupokea majukumu atayoachiwa na bossi wake huyo.

“Mimi nipo poa tu, tayari nimeshazungumza naye kuhusu ili swala na naamini kila kitu kitaenda sawa,” alisema Temba.

Pia Temba alisema hata kama akiwa kwenye jukumu la umeneja hataacha kufanya muziki kwa kuwa muziki ni sehemu ya maisha yake.

Bongo5

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364