-->

Matatu Kutoka kwa Mwana FA Baada ya Kuoa

Miezi kadhaa baada ya kuuaga ukapera, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ amefunguka mambo matatu ambayo hayafanyi tangu ameoa.

mwanafaw

KUPIGA MISELE
“Kwa kweli tangu nioe, imenibidi kupunguza baadhi ya ratiba ambazo zilikuwa zinanichukulia ‘time’ huko nyuma na kunifanya wakati mwingine kuwa nje ya nyumbani. Kwa kuwa mimi siyo mtu wa kujirusha kiivo, suala hili limekuwa rahisi na inanipasa kuwa karibu zaidi na familia.

KUONDOA MTAZAMO HASI JUU YA NDOA
“Kipindi cha nyuma nilikuwa ‘sometime’ nasikia kuwa mtu akioa hasa msanii kuna uwezekano mkubwa wa kupotea kwenye gemu, si kweli, mtazamo huo tangu nioe nimeuondoa kabisa kwa kuwa mke wangu ni mtu wa burudani na anafahamu ninachokifanya. Kikubwa ni kupanga ratiba juu ya mambo yangu na kujua nini natakiwa nifanye katika wakati husika.”

KUJISAHAU
“Kuna wakati unafika ukiwa mwenyewe tena mwenye mafanikio unaweza kujisahau na kuona kuwa umefika, mafanikio uliyoyapata yanatosha. Lakini ukweli ni kwamba kutokana na kuwa na familia inanibidi kufanya kazi kwa bidii, kwa kuwekeza kwenye muziki wangu na mambo mengine ili kuhakikisha familia yangu inapata kila kitu inachokitaka. Zaidi ni kuwaandalia maisha bora ya leo na kesho!”

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364