-->

Fid Q Atoa Sababu ya Kuvaa Koti Lililochanika

Msanii Fid Q ambaye ni rapa wa hapa Bongo kutoka pande za Rock City/Mwanza, ametoa sababu iliyomfanya akavaa koti lililochanika kwenye video yake mpya, na kuleta minong’ono kwa mashabiki.

fid-2

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Fid Q amesema aliamua kuvaa hivyo ili kuweza ku’relate na maisha halisi ya mashabiki, ambao asilimia kubwa wanashindwa kuhimili vitu vya gharama ambavyo wasanii wanavaa kwenye video zao, na kuhisi kutengwa.

“Unajua ni muda mrefu wanamuziki wamekuwa wakifanya video, wanavaa vitu ambavyo asilimia 90 ya mashabiki wao hawawezi kuvi’aford’, wanakuwa wanavitamani tu, lakini njia rahisi siku hizi ya kuweza kufikisha muziki ni kuhakikisha kwamba unafanya kitu ambacho wanaweza waka’relate’ nacho, wanaweza wakajihusisha nacho au kikawa kinawahusu”, alisema Fid Q.

Pia Fid Q aliendelea kwa kusema kuwa pamoja na kuamua kujihusisha na maisha halisi ambayo mtaa anaoishi yapo, aliamua kufanya hivyo kama moja ya mtindo wa nguo zake alizovumbua, akifananisha na ile mitindo ya msanii wa Marekani Kanye West.

“Hatupaswi sana kuwa tunajifanya ndo wasanii tunavaa vitu vya gharama zaidi, wakati tunawakilisha maisha halisi ya mitaa ambayo tunatokea, mitaa ninayotokea mimi kuna watu wanavaa majacket ambayo yameshavaliwa, yamechanika kwa sababu ya shida, kwa hiyo nawakilisha ninakotokea mimi, kwa hiyo ule ndio uhalisia na ndio fasheni ambayo nimeivumbua, kama ambavyo Kanye West amevumbua nguo zake”, alisema Fid Q.

Msikilize zaidi hapa akielezea sababu ya kuvaa koti hilo ambalo linaonekana kuchakaa na kuchanika.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364