-->

G Nako Afunguka Ishu ya Kulala Kwenye Jeneza

Rapa G Nako amefunguka na kusema kwamba ujumbe na lengo lake limefanikiwa baada ya watu kushtuka walipomuona  ndani ya jeneza kwenye video ya wimbo wake mpya ‘Luck Me’ huku akikumbusha kwamba kila mtu lazima aingie kaburini na kusisitiza ibada.

Rapa G Nako

G Nako amefunguka hayo mbele ya kamera za eNewz ya EATV baada ya kuzua gumzo mtandaoni ikiwa ni siku chache tangu video hiyo ianze kuonekana na kuweka wazi hofu ya wazazi wake ingawa kwa asilimia kubwa ametimiza malengo yake.

“Wazazi wameogopa lakini, yani kuna hofu fulani ila tumewaelewesha na wameelewa. Nilichojaribu kukifanya ni sanaa tulijaribu kuwa creative  na hakuna kingine ila asilimia nyingi wameelewa ila asilimia ndogo kidogo kama wameogopa na wamechukulia tofauti na jeneza lilikodishwa na watu wenye jeneza lao walikuwepo na baada ya kumaliza kulitumia walilichukua ili kwenda kulifanyaia kazi nyingine” G Nako alifunguka.

Aidha G Nako ameongeza kwamba “Vile watu waliposhtuka ndilo lengo letu lilipokuwa kwa maana ujumbe umefika. Pamoja na kwamba watu wameogopa wanatakiwa kukumbuka sote tutapitia hatua hiyo hivyo ukumbuke kufanya mema na kusali sana”

Rapa G Nako

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364