Vanessa Atoa Povu Jux Kumaliza Chuo
Msanii Vanessa Mdee amempongeza mpenzi wake Juma Jux kwa kuhitimu elimu yake ya juu nchini China huku akiwapiga vijembe wale waliokuwa wanamsema msanii huyo kuwa hasomi bali anakwenda kukunua nguo, na kwamba picha alizoweka leo ni jibu tosha.
Vanessa Mdee ametoa pongezi hizo ikiwa ni siku moja baada ya Msanii huyo kuhitimu, na kutupia kijembe kwa wale waliokuwa wanapiga kelele siku za nyuma katika mitandao na vyombo vya habari vikimtaka Jux athibitishe kwa picha akiwa darasani kama kweli anasoma huko, na kama jinsi wanafunzi wengine wafanyavyo wakiwa vyuoni.
“Congratulations Juma Jux finally done and you done did it well’. Hapo watu waliyokuwa wakiombaga picha za wewe darasani nadhani hii ni picha jibu la kutosha. Umeweza kufanya yote, muziki, biashara pamoja na shule, ‘now that’s exceptional’ muda wa vibunda baba. ‘Keep inspiring ” aliandika kupitia mtandao wake wa kijamii Vanessa.
Hata hivyo Jux mara nyingi amekuwa akitoa kauli ya kutothubutu kupiga picha kumuonesha akiwa darasani na kwamba yale ni maisha binafsi.
“Darasani sio sehemu ya kupiga picha umuoneshe mtu, kwanza darasani kwetu hairuhusiwi kupiga picha, haiwezekani kuwa mwalimu yupo anafundisha halafu napiga picha nioneshe watu, No. Mazingira yangu ya nje ya chuo nafanya kwavile ni maisha yangu ya nje ya chuo” Jux hukaririwa mara nyingi akitoa jibu hili kwenye vyombo vya habari.