-->

Gabo Afunguka Kuhusu Bifu

MKALI wa Filamu za Bongo, Gabo Zigamba, amesema wasanii kuendekeza bifu ni dalili za kujimaliza kabisa na kukosa ubunifu kwenye kazi zao.

Hivi karibuni msanii huyo amejikuta katika ugomvi na msanii mwenzake, Daudi Michael maarufu kama Duma kutokana na kila mmoja kumlalamikia mwenzie kushindwa kuitendea haki tasnia hiyo.

Gabo amesema kuendelea kuzozana na Duma ni kujidhalilisha, kwani kufanya hivyo ni kujimaliza zaidi katika kazi zao.

“Unadhani bifu kama hizi zinasaidia? nadhani ni kuendelea kujichimbia kaburi na kupotea kabisa katika ramani ya sanaa, tushindane katika kutoa kazi nzuri, zenye ubunifu kwa masilahi yetu na ya mashabiki,” alisema Gabo.

Gabo amekuwa akilalamikiwa na Duma kuwa ni mmoja wa wasanii ambao wanadidimiza tasnia ya filamu kutokana na kupewa hadhi kubwa ambayo kwa sasa inaonekana kumzidia.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364