-->

Gabo Ashushiwa Kipigo, Apoozwa kwa Msosi

STAA wa filamu za Kibongo Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ ametoboa kuwa, baba yake mzazi, mzee Ahmed alikuwa mkali sana, lakini kamwe hawezi kusahau siku alipochezea bakora za kutosha na mama yake akamtuliza kwa msosi.

gabo89

Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’

 

Akisimulia kisa hicho, Gabo ambaye amenyakua Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume kwa mwaka huu iliyotolewa na ZIFF, alisema kwa kawaida baba yake alipenda kuona watoto wake wote wakiingia ndani mara ifikapo saa 12.00 jioni jambo ambalo hakuwa akitimiza kutokana na kupenda sana kucheza mpira.

“Nilikuwa napenda sana mpira. Kama unavyojua tena watoto huwa hawana ratiba ya kueleweka ya michezo, mara nyingi nilikuwa nachezea kichapo. Lakini siku hiyo nilikuwa nimegombana na dada yangu, kwahiyo niliondoka zangu nyumbani kwenda mpirani.

“Nilirudi nikiwa nimechelewa, lakini pia sista alikuwa ameshanichongea kwa mzee. Nilikuta baba ameshaandaa bakora zake. Nilichapwa sana aisee. Nililia sana, mama akanionea huruma.

“Siku hiyo mama alikuwa amepika wali na maharage na unanukia kinoma. Mzee akaniambia hakuna kula, kiunyonge nikaingia zangu chumbani, lakini baadaye bi mkubwa aliniletea sahani ya wali, akasema pole sana baba, ila uache utundu,” alisema Gabo.

Akaongeza: “Nilikula kwa furaha moyoni, ingawa bado machozi yalikuwa bado hayajakauka. Sichukizwi na bakora za baba yangu, maana kiukweli bila yeye leo hii nisingekuwa hivi. Nidhamu niliyonayo ni kutokana na mzee kuwa mkali na mwenye msimamo.

“Lakini pia namshukuru sana mama yangu kwa moyo wake wa upendo. Kiukweli wamama huwa wanawapenda sana watoto wao, huwaonea huruma na kuwajali. Lazima tuwe karibu na mama zetu. Tuwakumbuke sana wazazi wetu.”

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364