-->

Gari ya Aunty Ezekiel Yashikiliwa na TRA

Gari ya mwigizaji wa bongo movie Aunty Ezekiel imeshikiliwa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), baada ya kutumia gari kabla ya kulipia ushuru.

aunty ezekiel34

Gari yake ya aina ya AUDI aliyoiagiza afrika kusini ilikamatwa mwezi mmoja uliopita ikiwa na namba ambazo siyo Tanzania.

Aunty Ezekiel ameeleza kuwa aliitumia gari hiyo wiki moja tu ndipo mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), wakamkatamata na kumtaka aonyeshe vibali vya gari kuruhusiwa kuingia nchini na akakutwa na vibali vyote.

Msanii huyo amedai kuwa hakujua taratibu za kulipia ushuru lakini kwa sasa ameshazijua na ametakiwa kulipia mamilioni kadhaa ya pesa kwa ajili ya ushuru na siku za karibuni atalipia ili gari yake itaachiliwa.

Gari

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364