Gigy Afunguka A-Z Kuhusu Picha Zake Chafu na Mwanasheria Msando (Video)
Baada ya weekend hii kusambaa video chafu ikimuonyesha mwanasheria nguli, Albert Msando akishikana shikana na video vixen, Gigy Money na kuzua taharuki mitandaoni, Gigy amefunguka kuzungumzia sakata hilo A-Z.
Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Gigy amedai wakati akirekodi video hiyo na kuisambaza mtandaoni mwanasheria huyo aliridhia.
“Jumapili hii nilienda Arusha na kile mlichokiona ilikuwa ni safari ya mimi nikitokea Moshi kwenda Arusha. Mimi nilitoka kwenye show Boma nikaenda Moshi kabisa baada ya kufika kama saa 12 asubuhi nikapokea meseji kutoka kwa Msando akiniambia nipo njiani nakuja Moshi kikubwa nataka nikuone, yaani kama shabiki yangu kwa sababu niseme ukweli mimi sijawahi kumuona hivi Msando hata wakati anakuja sikujua yukoje wala sijui anafanya ishu gani,” alisema Gigy.
“ Baada ya kufika hoteli kwetu kuna baadhi ya marafiki zetu wakawa kama wanakwaruzana nikasema mimi siwezi kukaa hapa, nikasema ngoja niende Arusha. Nikamwambia Msando umekuja kuniona ngoja tuondoke wote Arusha. Wakati tupo kwenye gari niliwa narekodi snap kama kawaida yangu haijawahi kuzima ina matukio mwanzo mwisho Wakati naendelea kurekodi nikauliza jamani naweza kurekodi? Yeye ndo wa kwanza na mimi nirekodi. Nikasema poa maskini ya Mungu sijui kama yeye ni nani, sijui kama ni mwanasheria,” aliongeza.
“Katika kurekodi kwangu mara nakuta ananishika shika, brand yangu mimi ni kuwa sex, nikasema kwaajili ya snap yangu ionekane kali ngoja tuendelee kurekodi kumbe haikuwa kawaida ilivyotoka nje. Lakini kama angeniambia yeye ni mtu fulani nisingefanya vile, nilifanya hivyo baada ya kugundua kumbe ni mpenda kiki mwenzangu,” alifafanua zaidi.
Gigy alisema baada ya kufika Arusha waliachana muda mchache baadaye na kila mtu aliendelea na mambo yake.
Alisema baada ya kufika jioni alianza kuona hali imekuwa tofauti baada ya kutumiwa video hizo kwa njia ya mtandao wa WhatsApp kutoka kwa watu wake wa karibu.
Hata hivyo Gigy alidai wakati kukio hilo likiendelea, mwanasheria huyo hakuonyesha dalili yoyote ya kuwa na wasiwasi.
Baada ya video hizo kusambaa mitandaoni na watu kushangazwa na tukio hilo kutokana na hadhi ya mwanasheria huyo, Msando aliamua kuwaomba radhi ndugu,jamaa na marafiki pamoja na mashabiki wake.
“Nikikaa kimya nitakua mnafiki. Nimekosea. Kilichotokea hakikupaswa kutokea. I will be a man enough and say sorry kwa wote ambao nimewakwaza na kuwaangusha. Am so sorry. But the beauty of all this is we all are human. Kuna watu ambao wamekuwa wepesi kuhukumu. Siwalaumu. Ni sawa na ni haki yao. I made a stupid mistake. I take full responsibility. Mwisho wa siku maisha lazima yaendelee. It could have been worse. And to all those who took time to text I appreciate. Thats friendship. #TheDon #Hennessy #TheClip” aliandika Msando kupitia Instagram.
Pia mwanasheria huyo ameonekana akipost video mtandaoni akiwa na mke wake akionyesha yupo sawa na mama watoto wake hicha ya tukio hilo kuitingisha familia yake.
Bongo5