Madam Flora Afunguka Haya kwa Mume Wake
Msanii wa nyimbo za injili nchini, Madam Flora amefunguka na kusema mume wake wa sasa Daudi Kusekwa ni mwanaume shujaa kwani ni mtu aliyevumilia mengi.
Madam Flora alisema hayo siku ya kuzaliwa kwa mume wake huyo ambayo ilikuwa Jumapili huku akimtakia maisha marefu na mafanikio mema
“Hongera mume wangu Daudi Kusekwa kwa kuzaliwa, Mungu akupe maisha marefu na yenye amani na furaha tele. Wewe ni mwanaume shujaa, nakupenda sana Daudi wangu na ninakuombea ufanikiwe zaidi kiroho na kimwili. Furaha yako ni furaha yangu” aliandika Flora.
Kwa upande wake Daudi Kusekwa aliitumia siku hiyo pia kumshukuru Madam Flora na kudai amepata mke mwema mwenye mapenzi ya dhati na yeye
“Napenda kumshukuru Mungu wangu kwa kunipa mke mwema na mzuri, anayenipenda kwa dhati”- alisema Daudi Kusekwa