-->

H Baba: Viongozi wa Simba Wananihitaji Nichezee Simba

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva H Baba amefunguka na kusema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa Simba wameonesha nia ya kumuhitaji kwenye kikosi chao.

H baba (kulia) akiwa na Kaburu (Kushoto)

H baba (kulia) akiwa na Kaburu (Kushoto)

H baba ambaye alikuwa nahodha wa timu ya soka ya Bongo Fleva ambayo ilipambana na timu ya Bongo Movie katika mchezo wa hisani uliochezwa mwishoni mwa wiki hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, amesema neema hiyo ni kutokana na uwezo aliouonesha katika mchezo huo.

H Baba baada ya kuingoza vyema timu ya Bongo Fleva na kuibuka na ushindi wa bao 6 dhidi ya 5 alisema alipata nafasi ya kukutana na moja ya kiongozi wa Simba ambaye alionesha kukubali uwezo wake.

“Baada ya ushindi dhidi ya Bongo Movie nilikuwa na kiongozi wa Simba Kaburu tukiongea mawili matatu, kaniuliza ‘kwa mpira niliocheza leo (Juzi) na mabao mazuri niliyopachika juzi upo tayari kutua Simba dirisha dogo? ” aliandika H Baba kupitia ukurasa wake wa Instgram.

Mbali na hapo H Baba alizidi kuonesha kuwa huenda Wekundu wa Msimbazi wamevutiwa na uwezo wake kwani baadaye alikuja wauliza mashabiki wa Simba kama wataweza kumpokea katika klabu hiyo na kuwaahidi kutupia mabao kila mechi.

“Namshukuru sana Mwenyezi Mungu na timu nzima ya Bongo Fleva kwa kuniamini na kunipa unahodha huu, na kuipatia timu yangu ya Bongo fleva ushindi mnono wa goal 6-5 baada ya mikwaju kumalizika dhidi ya Bongo Movie. Je, mashabiki wa Simba mtanipokea Msimbazi? kila mechi Taifa nafunga siyo chini ya bao mbili mbili kwa timu tofauti tofauti” alindika H Baba.

eatv.t v

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364