Makonda Awashukuru Mastaa Wanaoiunga Mkono Kampeni ya ‘Mti Wangu’
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa shukrani kwa muigizaji Jacqueline Wolper na wengine wanaoiunga mkono kampeni yake ijayo, Mti Wangu.
Mkuu wa mkoa huyo ametoa shukrani zake katika ukurasa wake wa Instagram kwa kuweka picha ya muigizaji akiwa amevaa t-shirt yenye logo ya neno ‘mti wangu’ akionesha juhudi za kumuunga mkono.
“Huwezi kujua umeugusa kwa kiasi gani moyo wangu, wewe na wote wanaosupport campaign yangu ya ‘MTI WANGU’ ninawashukuru sana sana”, aliandika Makonda.
“Endeeleni kuiunga mkono serikali, kwani miti tunayoipanda ina faida kubwa sana kwetu sisi wananchi”, aliongeza.
Mkuu wa mkoa alisema kampeni ya upandaji miti utakuwa Oktoba Mosi mwaka huu.
BY: EMMY MWAIPOPO
Bongo5