-->

VIDEO:Mwana FA Afunguka Haya Kuhusu Mchango wa Prof Jay Kwenye Bongo Fleva

Mwana FA anataka kuweka mambo clear: Hakuna mtu mwenye mchango mkubwa kwenye muziki tunaofanya kama Profesa Jay.

Ameiambia Bongo5 kuwa huo ni ukweli ambao wachache wasiompenda watapinga hadharani lakini mioyoni mwao wana msimamo tofauti.

“Mimi binafsi ni heshima ya kipekee kabisa kwa Profesa Jay. Hakuna mtu mwenye mchango mkubwa kwenye aina ya muziki tunaofanya kama Profesa Jay. Mtu yeyote ambaye hukumbuki hata wimbo wake mmoja probably akaja akamkosoa Profesa Jay kwasababu amefanya Singeli sio sawa,” anasema FA.

“Kutopenda muziki wa mtu sio shida, lakini kuwa disrespectful ndio kitu ambacho sikitaki. Mimi binafsi pengine sipendi Singeli ya Profesa kama nilivyopenda Bongo Dar es Salaam, kama nilivyopenda jina langu, lakini siwezi kusema Profesa anachemka, ‘huu ni up*mbavu’ kuna maneno makali zaidi yalitumika hata siwezi kuyataja kwa heshima niliyomwekea,” amesisitiza.

“Watu wanaweza wakawa na decency kiasi fulani, na heshima kwa kiwango fulani halafu na ukatoa makemeo kuhusiana na muziki ambayo hayatokuja na ukosefu wa adabu.”

Hivi karibuni Nash Mcee alijikuta akikosolewa vikali kwa kumkejeli Profesa Jay kuhusiana na kauli yake ya kuupeleka muziki wa Singeli kimataifa.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364