-->

Wasanii Wamtenga Shija, Afunguka Mazito

STAA wa sinema za Kibongo, Deogratius Shija amefunguka kuwa, wasanii wanamtenga, kisa sakata la unga ambalo lilimsababishia kuwekwa sero bila kujua sababu ya yeye kuingia huko.

Deogratius Shija

Akizungumza na Amani baada ya kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam alikowekwa sero kwa siku 15, Shija alisema katika sakata hilo ambalo lilihitaji faraja ya wasanii wenzake, hakuna aliyemtembelea zaidi ya mwigizaji William Mtitu aliyemfariji kwa kumpelekea maji na sabuni.
“Sasa nimejua ndugu na rafiki wa kweli. Ninamshukuru Mtitu maana yeye tu ndiye alijitolea kuniona bila kujali nimefanya au sijafanya,” alisema Shija.

Akisimulia mkasa mzima wa kukamatwa kwake, Shija alisema kuwa, anakumbuka ilikuwa usiku wa Februari 9, mwaka huu ambapo askari walifika nyumbani kwa rafiki wa Shija aliyemtaja kwa jina moja la Liberty, wakiwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa kisha kuwakamata.

Alisema askari hao walisema kuwa walikuwa wakimsaka rafiki wa jamaa aitwaye Mwinyi Machapta waliyemtaja kwa jina la Liberty. “Walipofika walituchukua hadi ‘Sentro’ wakatusweka ndani kwa siku 15.

Sikuhojiwa kwa lolote zaidi ya kujieleza na baada ya hapo, walinirudisha sero wakanifungulia faili la uchunguzi, walichukua simu lakini hadi leo siwezi kukuambia nimekosa nini ila nilikamatwa kwa sababu ya rafiki yangu, Liberty kwani ninaishi naye,” alisema Shija.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364