Hakuna Zaidi Yangu – Chid Benz
Rapa Chid Benzi amefunguka na kusema kwa Tanzania hii hakuna msanii mkali kama yeye na hatatokea msanii ambaye anaweza kuchukua nafasi yake kwa mashabiki wake sababu hata hao mashabiki zake wanatambua kuwa hakuna msanii mkali zaidi ya Chuma.
Chid Benzi amesema hayo alipokuwa akiwatoa hofu watu juu ya yeye kurudi kwenye muziki na kusema muda wowote kuanzia sasa na dakika yoyote atarudi kwenye muziki kwani tayari ameshamaliza muda ya kukaa rehab na toka ametoka huko saizi ni miezi miwili imeshapita na afya yake inaendelea vyema.
“Mashabiki wangu mimi wapo tu kwani mimi nina njia yangu, kwa hiyo watu wangu mimi hawasaliti hata uwashikie risasi na wanajua kwamba Chid yupo na ni mkali ambaye hakuna mkali mwingine ambaye amewahi kutokea katika hii nchi na mtakua naye mkali kama mimi, kwa hiyo dakika yoyote na muda wowote nitarudi kwenye muziki mashabiki wangu na watu wangu nitakuwa nao” alisema Chid Benz
Mbali na hilo Chid Benz anakiri kuwa kweli aliwakosea watu wengi ambao walionyesha nia ya kumsaidia na kusema kama binadamu aliteleza lakini saizi yuko poa anajitambua hivyo anaamini atafanya kazi na watu hao hao, na kusema muda wowote atarudi na kudondosha ngoma.
eatv.tv