-->

Harmorapa Amjibu Afande Sele

Wiki iliyopita Mfalme wa Rhymes nchini Tanzania, Afande Sele alizungumzia hali ya muziki ilivyo kwa sasa na kwenye mazungumzo hayo alisikika akisema hajui ngoma yoyote ya Harmorapa na hata kwa mara ya kwanza kumuona ni pale alipotokea kwenye tukio la Nape kushikiwa Bastola, hivyo haelewi muziki anaoufanya zaidi ya kumuona mitandaoni tuu. Hatimaye Harmorapa amemjibu.

 

Harmorapa amemjibu Afande Sele kwa kusema, yeye hana muda wa kujibizana na mtu bali anaacha kazi zake ndiyo zimjibu Mfalme huyo wa Rhymes, huku akimuasa kuwa hakuna Msanii ambaye alianzia juu kwani hata yeye alianzia chini.

Niseme tuu yeye kwanza mwenyewe akae chini na kujua na kukumbuka kuwa alianzia chini mpaka kufika level fulani watu wakamkubali “Aliendelea kumuonya Afande Sele kwa kusema

Ajue mimi kama Harmorapa sina maneno mengi ila kazi zangu ndiyo zitakuja kumuelekeza kuwa Harmorapa uliyekuwa unamuongelea ndiyo huyu kupitia kazi yangu ndiyo itakuwa imemnyoosha au vipi? na  ku’prove ukali wa Harmorapa “Alisema Harmorapa kwenye mahojiano yake na EATV.

By Godfrey Mgallah

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364