-->

Hamisa Mobetto Kuibuka Ndani ya Zero Player

MWANAMITINDO Hamisa Mobetto, anaratajia kuonekana kwenye filamu mpya ya ‘Zero Player’ itakayozinduliwa Novemba 17 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA, kiongozi wa filamu hiyo, Allan Upamba, alisema Zero Player ambayo imefanyika nchini Afrika Kusini na kuchezwa na wasanii maarufu wa ndani na nje ya Tanzania, itazinduliwa rasmi kwenye Ukumbi wa Suncrest Cineplex Cinema uliopo Quality Centre, Barabara ya Pugu.

“Zero Player inakuja kufanya mapinduzi ya soko la filamu ambapo ndani yake kuna mastaa wengi, ila Hamisa Mobetto ametikisa kwa kucheza kiwango cha juu kiasi kwamba natamani kila Mtanzania aone uwezo wake, imeongozwa na mwongozaji mkubwa Afrika Kusini aitwaye Holger Sconfeld na ujumbe ukiwa ni matukio yaliyotuzunguka kila siku, kwa hiyo watu waje siku hiyo tuizindue pamoja,” alisema Upamba.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364