-->

Harmonize: Mapenzi Yetu na Wolper Sio ya Kiki

Harmonize amefunguka kuwa ni kweli waligombana na mpenzi wake Jacqueline Wolper na haikuwa kiki kama watu wanavyofikiria.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatano hii, kuna baadhi ya vitu vilisababisha wagombane lakini kwa sasa kila kitu kinaenda sawa.

“Kuna vitu vilitokea tukajikuta hatuko sawa, lakini Mungu ndio mwenye kheri tukawa tupo pamoja tukajua kabisa kuwa hiki kitu Jack hakipendi au mimi. Sasa hivi kila kitu kinaenda sawa na mapenzi yetu sio ya kiki, nafasi yetu kwenye jamii imefanya ionekane kuwa ni kiki,” amesema Harmo.

Hitmaker huyo wa Matatizo ameongeza kuwa alianza kuwa na mahusiano na Wolper muda mrefu tangu kipindi hana gari anatembea kwenye bajaji.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364