-->

PICHA & VIDEO: Rais Magufuli Alivyotembelea Eneo la Ujenzi wa Ikulu Chamwino Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo March 16 2017 ametembelea eneo la ujenzi wa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma na kuwahakikishia wananchi kuwa atahamia Dodoma hivi karibuni kama alivyoahidi.

Rais Magufuli ambaye ameongozana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenister Joakim Mhagama na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema pamoja na majengo ya Ikulu Serikali itajenga miundombinu mingine zikiwemo reli na barabara za lami zitakazounganisha maeneo ya vijiji vinavyozunguka Ikulu na mji wa Serikali.

Aidha Rais Magufuli amewahakikishia wananchi kuwa wote watakaoguswa na shughuli za ujenzi wa miundombinu ya Serikali na
wanaostahili kulipwa fidia watalipwa, na ametoa wito kwa wananchi hao kutumia fedha za fidia watakazolipwa kujenga makazi bora na kujipanga kufanya shughuli zenye manufaa kwao.

“Hapa sasa watakuja watu wengi, wafanyakazi na wageni maana tayari Mabalozi wa nchi mbalimbali nao watajenga ofisi zao hapa, sasa na nyinyi mjipange kufanya biashara, mtapata soko la kuuza mazao na bidhaa nyingine, mkipata fedha ziwasaidie kwa manufaa na sio kuzichezea”-Rais Magufuli

Rais Magufuli na wahandisi na maafisa wa Wakala wa Majengo ya Serikali
Sehemu ya matofali katika eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino
Unaweza kubonyeza play hapa chini kutazama Rais Magufuli alivyotembelea eneo la ujenzi wa Ikulu Chamwino Dodoma


MillardAyo.com

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364