Harmorapa Afungukia Uhusiano Wake na ‘Wolper Feki’
Msanii chipukizi wa Bongo Fleva anayefanana sana kwa sura na msanii kutoka WCB, Harmonize kiasi cha kubatizwa jina la ‘Pacha wa Harmonize’, Harmorapa, leo ametinga kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga- Mwenge jijini Dar ambapo mbali na mambo mengine, amefungukia uhusiano wake wa kimapenzi na ‘Wolper’.
Harmorapa amesema kuwa kutokana na kufanana sana na Harmonize, aliamua kutafuta msichana anayefanana sana na mpenzi wa Harmonize, mwanadada Jacqueline Wolper ambaye naye kwa jinsi anavyofanana naye, ukikutana nao unaweza kudhani umekutana na Harmonize na Wolper ‘orijino’.
“Prodyuza wangu, Khalfan ndiye aliyenikutanisha na mwanadada huyu ambaye watu wanamuita Wolper kutokana na jinsi alivyofanana naye, alinikutanisha kwa lengo la kufanya naye kazi akiwa kama video queen, akatokea kuwa rafiki yangu sana na mara kwa mara nakuwa naye sehemu mbalimbali.
“Kiukweli uhusiano wetu ni wa kikazi tu tofauti na Harmonize na Wolper ambao ni wapenzi kweli.”
Chanzo:GPL