Ray Kigosi: Chuchu Amenifanya Niitwe Baba, Abandika Picha ya Mtoto Wake
Hatimaye Staa wa Bongo Movies, Vicenti Kigosi ‘Ray’ amejitokeza na kumwagia pongezi mpenzi wake wa muda mrefu chuchu Hans kwa kumzalia mtoto.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram, Ray amefunguka haya;
Asante Mungu kwa kuniletea pacha wangu asante my lovely mzungu kwa kunipa heshima kubwa kunifanya niitwe baba, Mungu wangu wa haki asiyeshindwa na jambo akubariki sana …… sasa msianze maneno yenu kwamba mwanangu amekunnywa maji mtoto bado ni mchanga maana watu wa insta kiboko lakini hawaishi mtoni.
Hongera sana Ray na Chuchu