-->

Harmorapa Aibuka, Aahidi Kuja na Drama Zaidi

Dar es Salaam. Baada kuwa kimya kirefu msanii Harmorapa aemeibuka na kusema mashabiki wake watarajie drama zaidi ya zile za mwaka jana.

Msanii huyo asiyeishiwa vituko, alikuja juu kipindi cha mwaka jana baada ya kufananishwa na msanii anayefanya vizuri katika muziki wa bongofleva Harmonize anayemilikiwa na kundi la wasafi.

Akizungumza na Mwananchi jana Ijumaa, Harmorapa amesema alikuwa kimya kwa muda akijipanga namna ya kurudi upya ambapo mbali na kuendeleza muziki wake anatarajia kuwa na drama nyingi kuliko za mwaka jana.

Akizungumzia kuhusu hali anayopitia baada ya kutoswa na meneja wake, Irene Sibuka amesema imemfanya kufanya vitu vingi mwenyewe na ni moja ya sababu pia iliyomfanya awe kimya.

“Hata hivyo nashukuru kutokana na tayari kuwa na jina kuna baadhi ya maeneo nikifika mambo yanaenda harakaharaka, hivyo pamoja na kutofautina na meneja wangu kiukweli sitakaa nimsahau kwa kuwa yeye ndio kanifikisha hapa,” amesema Harmorapa.

Kwa upande wa kazi zake za muziki, amesema tayari ana nyimbo kibao na anachohangaikia kwa sasa ni kupata wadhamini wa kumsaidia kuingia studio.

Mpaka sasa Harmorapa alishatoa nyimbo tatu ikiwemo usigawe pasi, kiboko ya mabishoo na ajitokeze.

Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364