-->

Waziri Mwakyembe Amtembelea Wastara

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe hapo jana( Jumapili) alikwenda kumtembelea msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma nyumbani kwake na kumjulia hali.

Mh.Waziri Mwakyembe ambaye aliambata na Katibu wa Bodi ya Filamu walifika nyumbani kwa muigizaji huyo kwa ajili ya kumjulia hali ambapo Waziri huyo aliahidi kumsaidia kiasi cha shilingi milioni. 1 kwa ajili kwenda India kwa ajili ya matibabu yake.

Hata hivyo Waziri Mwakyembe amewaomba wasanii wote nchini kuwa na moyo wa kujitolea na kumsaidia Wastara Juma ambae anahitaji kiasi cha shilingi milioni37, kwa ajili ya kurudi katika hospitali aliyokuwa akitibiwa hapo awali .

Kitendo cha Mh,Waziri kufika nyumbani kwa muigizaji huyo kimekuja baada ya msanii huyo kuomba msaada kutokana na hali yake hiyo baada ya kupata ajali ya pikipiki miaka kadhaa iliyopita na kumsababisha kukatwa mguu.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364