-->

Harmorapa Arushiwa Chupa Stejini

Msanii Harmorapa ambaye anafanya vyema na wimbo wake ‘Kiboko ya mabishoo’ jana usiku kwenye usiku wa Komela alijikuta katika wakati mgumu baada ya moja ya shabiki aliyekuwepo katika show hiyo kumrushia chupa akiwa stejini.

Harmorapa akiwa na meneja wake Irene Sabuka

Harmorapa ambaye katika show hiyo alitokea kama mgeni mwalikwa, alipata nafasi ya kuwasalimu mashabiki wake na kufanya show kidogo lakini wakati rapa huyo akifanya yake stejini alijitokeza kijana mmoja na kurusha chupa huku akiwa na lengo la kutaka kumpiga msanii huyo.

Harmorapa ni kama aliwahi kuiona ile chupa na kubahatika kuikwepa hivyo haikuweza kuleta madhara ya moja kwa moja kwa msanii huyo ila sauala hili lilipelekea msanii huyo kushindwa kuendelea kufanya show.

Akiongea kwenye Planet Bongo meneja wa Harmorapa Irene Sabuka alifunguka na kusema kama Harmorapa asingeweza kukwepa ile chupa au kwa bahati mbaya ingemkuta saizi huenda tungekuwa tunazungumza mambo mengine.

“Kiukweli hili jambo la kusikitisha sana, Harmorapa alikuwa stejini ana perfom ila kabla ya kumaliza show alitokea mtu mmoja akarusha chupa stejini bahatai nzuri Harmorapa akakwepa ile chupa, laiti asingekwepa au ingemkuta kwa bahati mbaya saizi tungekuwa tunazungumza mengine, mimi naona kile kitendo ni wivu tu sababu watu hawajui maisha kila mtu ananamna yake anayotokea, Harmorapa ametokea mtaani anatafuta maisha yake leo anaibuka mtu anamrushia chupa na kutaka kumjeruhi, anaibuka mtu mwingine anasema kuwa anataka kumuonyesha na kukomesha” alisema Meneja wa Harmorapa 

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364