-->

Harmorapa Awajabu Wanaomtafuta

Msanii ambaye hakauki vituko mitandaoni Harmorapa, amewajibu watu wanaomsema kuwa amepotea pamoja na kiki zake zote, na kusema kwamba hajapotea isipokuwa yuko busy na biashara.

Harmorapa ameyasema hayo leo kwenye eNewz ya East Africa Television, na kusema kwamba watu wanatakiwa wajue licha ya muziki Harmorapa ana maisha yake mengine ambapo pia ni mfanyabiashara, na sasa hivi yuko busy na kazi za biashara ikiwemo kusafiri, lakini mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani muda si mrefu atawapa kazi mpya.

“Watu waelewe sipo kimya, sasa hivi nipo busy na biashara nasafiri sana, ile kuonanana tu ni bahati,  project zangu za muziki zinaendelea kama kawaida wiki ijayo naachia dude jipya, watu wajue tu mimi nipo, wamemzoea Harmorapa leo kafanya hiki mara hiki, sasa hivi niko busy na muziki wangu bado upo, kama kutrend kila siku natrend, naingia Instagram nakuta tu mtu amenipost bado machoni mwa watu naonekana, bado mimi nipo na nitakuwepo na vitu vitaendelea”, amesema Harmorapa.

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwamba msanii huyo ameshapotea kwenye game, kwani hawezi kufanya muziki na anachotegemea yeye ni kiki ambazo anazifanya na kuchekesha watu.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364