Shamsa Ford Amtia Moyo Lulu
ALHAMISI wiki hii kesi inayomkabili staa wa filamu za kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayedaiwa kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, Aprili mwaka 2012, ilianza kusikilizwa tena kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam huku mashahidi mbalimbali wakitoa ushahidi wao.
Moja ya mastaa waliomtia moyo, Lulu ni Shamsa Ford ambaye alimtaka mrembo huyo kuwa mvumilivu katika kipindi hiki kigumu kwani ndiyo changamoto za maisha na zinaonyesha ukubwa.
“Changamoto tumeumbiwa binadamu na huwezi kujiita mkubwa kama hujapitia changamoto yoyote kwenye maisha. Mungu akusimamie mdogo wangu, Nothing is permanent in this world. @elizabethmichaeloffici,” aliandika Shamsa Ford kwenye Instagram chini ya picha inayomwonyesha Lulu akiwa na mama yake kwenye Mahakamani.
Mtanzania