-->

Hatimaye Shilole Kuolewa Sasa

Msanii wa bongo fleva asiyekaukiwa drama Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amedai kwa sasa ameshatolewa barua na mpenzi wake aliyeko naye kwenye mahusiano na endapo Mungu akimjalia atafunga naye ndoa ili kuhalalisha.

Zuwena Mohamed ‘Shilole’

Shilole amefunguka hayo kwenye 5Selekt ya  EATV na kusema kwa sasa ameamua kuweka mahusiano yake faragha kidogo ili aweze kuwa huru na mpenzi wake.

“Mimi kwa sasa hivi sina boyfriend kabisa, niwaambie tu nina mchumba ambaye tayari ameshanitolea mpaka barua, Mungu akijaalia harusi nitawakaribisha siku siyo nyingi.  Na kuhusu wapenzi waliopita kuwa na mahusiano na marafiki zangu naona ni kitu cha kawaida kwa sababu naamini mapenzi ni kama daladala ukishuka mwenzako anakaa” alisema Shishi.

Kuhusiana na muziki wake msanii huyo amedai anashindwa kutoa wimbo mpya kutoka na akaunti yake ya mtandao wa instagram kudukuliwa na wahalifu wa mtandao.

“Nina miezi mitano tangu nimeachia wimbo wa hatutoi remix najua masabiki zaingu wamenimiss sana lakini kinachonifanywa nishindwe ni kuwapa taarifa mashabiki zangu. Dunia sasa ipo mikononi mwa watu na kwa wasanii inatusaidia kusukuma kazi zetu ” aliongeza

Kuhusu kolabo za kimataifa “Zipo nyimbo nyingi na nahitaji kuzitoa kwenye mpangilio mzuri siyo kutoa tuu nataka nitoe heavy song kila mmoja asubiri” alimaliza

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364