Hawa Ndiyo Wasanii Watano Anaowakubali Shilole
Msanii Shilole ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake ‘Sitoi kiki’ amefunguka na kuwataja wasanii watano wa bongo fleva ambao yeye anawakubali na kupenda kazi zao.
Shilole alifunguka hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema katika wasanii hao msanii wa kwanza kabisa anayemkubali ni Bi. Khadja Kopa
“Jamanii mimi nampenda sana huyu mama Khadja Kopa, nampenda sana sana lakini mbali na huyo pia napenda kazi za msanii Linah Sanga, Mwasiti, Diamond Platnumz pamoja na huyo kijana huyu ambaye ameniimba, anaitwaa RayVanny” alisema Shilole
Mbali na hilo Shilole anasema hakubatika kwenda kwenye harusi ya Nuh Mziwanda sababu alikuwa na mishe zake zingine lakini amedai siku ya arobaini ya mtoto wake atakwenda kumuona mtoto na kumpa pongezi kwa kubarikiwa kupata mtoto.