-->

Hii ya Wolper kumkana Hamornize kali

SIKU chache baada ya kusambaa kwa kipande cha video kinachomwenyesha mwigizaji Jackline Wolper, akitoa onyo kuwa anapozungumziwa mwanamuziki, Hamornize, basi yeye asihusishwe kwa kuwa wameshaachana, mlimbwende huyo amezua jipya.

 

Wolper

Katika video hiyo Wolper anasikika akisema hataki kuzisikia habari za Harmonize kwani kwa sasa ana maisha yake, sasa bwana kumkana huko wala sio ishu, ishu ni namna Wolper alivyomtaja Harmonize akitumia jina la ‘Yule Kijana’ kwa maana kwamba amelisahau hata jina la X wake huyo.

Neno kijana ambalo Wolper amelitumia kumtambulisha Hamornize, ndiyo limekuwa gumzo la wiki. Kuna sehemu amemwita ‘yule mvulana’.

Katika video hiyo, Wolper anasikika akisema: “Unajua niwaombe kitu kimoja, msinishirikishe na habari za yule kijana kwani nimeshaachana naye na miezi imeshapita, hivyo mnavyokutana naye msimuulize habari za Wolper kwani kuna vitu vingi sana vya kumuuliza yule nani yule…. yule mvulana.”

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364