-->

Hip Hop si Dini Wala si Kabila- Darassa

Rapa anayefanya vizuri na wimbo wake wa ‘Too Much’ kwenye muziki wa bongo sasa Darassa amefunguka na kusema kuwa muziki wa Hip hop si kabila wala si dini ila yeye anatambua kuwa anakipaji.

darasa732

Akiongea kwenye kipindi cha ‘Ngazi kwa Ngazi’ kinachorushwa na EATV Darassa amesema watu wamekuwa wakiongea mengi juu ya muziki anaofanya, watu wamekuwa wakiongea mambo mengi ambayo hata wao wenyewe hawayajui ndiyo maana aliandika wimbo wa ‘Too Much’ kwa watu kama hao.

“Kwenye maisha huwa hawakosekani watu ambao wanaingia kwenye mishe zako, hao ndiyo watu ambao wanasababisha vitu kama ‘Too much’ itokee watu wanasema sijui huyu jamaa ni kwanini watu wanampenda mbona hatuoni kama hata anafanya Hip hop, wewe unaongelea Hip hop kama nani? Unajua nini kuhusu Hip hop? Mimi nafikiri braza ungekaa tukomalie muziki wa Saida Karoli chambua kama Karanga ndiyo tuseme huu muziki wetu, unajua nini kuhusu Hip hop, Hip hop imetoka mbele sisi tuko Tanzania Hip hop si kabila, Hip hop si dini mimi na talent, ‘people talk to much'” alisema Darassa

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364