-->

Mrembo Nakufa Kwa Ukimwi, Amtumia Ujumbe Aunty Lulu

Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kuwa ni muumini wa kanisa mojawapo jijini Dar, anayeshirikiana na wenzake kufanya maombi nyumba hadi nyumba, wamekutana na mrembo aliyekataa kumtaja jina maeneo ya Kawe, akiwa hoi akidai anakufa kwa Ukimwi, lakini akataka wafikishe ujumbe wake kwa msanii wa filamu, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.

auntlulu

Msanii wa filamu, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.

Akizungumza kwa njia ya simu aliyopiga chumba chetu cha habari, mwanamke huyo alisema kuwa mrembo huyo akiwa hoi alimtaka amfikishie A u n t y Lulu ujumbe kuwa atulie, kwani waliwahi ‘kushare’ mwanaume mmoja aliyewapa fedha nzuri na
ndiye aliyemwambukiza mrembo huyo gonjwa hilo la Ukimwi.

“Nimeshindwa kumpata Lulu, ila huwa naona magazeti yenu mkimwandika kila wakati, naomba mumfikishie ujumbe kuwa kuna dada ambaye ni rafiki yake, waliishi pamoja maeneo ya KinondoniMkwajuni, kwa sasa yupo hoi huku Kawe ndanindani, kuwa asiendelee kubadili wanaume, atulie. “Mrembo huyo anasema walitembea na mwanaume mmoja na Aunty Lulu ambapo huyo mwanaume aliwapa fedha nyingi lakini hawakuweza kufanya kitu cha maana na huyo ndiye aliyemwambukiza na tayari alishafariki, hivyo msanii huyo awe makini, akisema mwenzake aliona ni vyema amfikishie ujumbe huo kabla hajafa maana kwa  sasa hawezi kumpata,” alisema sista huyo.

Baada ya kupata ujumbe huo kutoka kwa sista ambaye hakutaka kutaja jina lake, wala kuelekeza sehemu alipo mrembo huyo na jina lake kamili, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Aunty Lulu ambaye alisema hamfahamu mrembo huyo na hajawahi kuishi na mtu yeyote Kinondoni-Mkwajuni zaidi ya aliyekuwa mpenzi wake, Bond Suleiman.

“Huyo mrembo simfahamu na hata kama tulitembea na mwanaume mmoja, atajuaje kama nilitumia kinga? Kila wakati huwa napima afya yangu na mara nyingi naenda na mama yangu na niko safi sina tatizo lolote. “Nahisi kuna mtu anataka kunichafua jina langu na mpenzi wangu wa sasa, Gasper kaniambia kuna mwanamke ambaye alimmwaga ndiye anayefanya hivyo maana ingekuwa ni kweli mrembo huyo asingeficha jina wala eneo analoishi ili nikamuone kama kweli alikuwa ni rafiki yangu,” alisema Aunty Lulu

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364