-->

Hivi Ndivyo Ndoa ya Nuh Mziwanda na Nawal Ilivyovunjika

Msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda ambaye hivi karibuni kumeibuka minong’ono kuwa ndoa yake na Nawal imesambaratika, amefunguka kuhusu hilo na kukiri kuwa kweli ndoa hiyo imekufa bila talaka, huku mke wake akiwa mbioni kuolewa na mtu mwingine.

Nuh Mziwanda amefunguka kuwa mke wake huyo hajampa talaka lakini ameolewa na mtu mwingine, huku vuguvugu kubwa lilianza kwa wakwe zake (wazazi wa mke wake)

“Mimi na Nawal tulitengana tu, lakini baada ya hapo kumbe mwenzangu ameshaandaliwa mume wa kumuoa, mimi baada ya kugundua hilo nikaona bora nirudi kwenye dini yangu, kwa hiyo wazazi wa mke wangu walikuwa wanajua kuwa mtoto wao ananisaliti”, alisema Nuh Mziwanda.

Nuh ambaye aliwahi kuwa kwenye mahusiano na msanii mwenzake Shilole, alipoulizwa kama alitoa talaka kwa mke wake huyo kama sheria ya ndoa inavyotaka watu wanapoachana, Nuh alisema hajatoa talaka na hawezi kutoa kwani tayari Nawal mke wa mtu.

“Mimi sijatoa talaka, na kufuatilia suala la talaka itakuwa kama najichoresha kwani wao wazazi wanajua kabisa kama ni mke wangu lakini wao wakaamua kumuozesha kwa mtu mwingine, kwa hiyo mimi naacha tu, mimi nitaangalia utaratibu wa kumlea mwanangu kwani bado mdogo hivyo bado yuko na mama yake”, alisema Nuh Mziwanda.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364