-->

Ndikumana Amfungukia Irene Uwoya

Mcheza mpira kutoka Rwanda Hamad Ndikumana ambaye ni mume wa muigizaji wa filamu za bongo Irene Uwoya, amekubali kumpa talaka Irene ili andelee na maisha yake baada ya kutengana muda mrefu huku akieleza kuchoshwa na skendo chafu za mke wake huyo.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Ndikumana ameandika ujumbe akisema amekubali kumpa Irene talaka, hivyo asisubiri hadi afe ili aolewe, ili ampe uhuru anaouhitaji aweze kufanya mambo yake bila yeye kuhusishwa.

“Ulilia muda kwamba unataka talaka ili uolewe, sina kipingamizi tafuta kila utakacho ulete nitakusainia, usisubiri nife ili uolewe maana naweza kuishi zaidi ya unavyofikiria, Mungu akusimamie”, aliandika Ndikumana.

Pia Ndikumana amesema kitendo cha Irene kumnyima kuzungumza na mwanae tangu watengane, ni kitendo kinachomuumiza sana, lakini yote anamuachia Mungu.

“Ungekuwa na roho ya kibinadamu ungekuwa unataka hata niwasiliane na mtoto, ila miaka miwili hujawahi chukua simu unipigie umpe mtoto niongee naye, hata picha tu hutaki nitumia ila naelewa kwa nini unafanya hivyo, na baada ya yote haya hutotaka nimuone tena, lakini ni sawa Mungu yupo na ipo siku”, aliendelea kuandika Ndikumana.

Irene na Ndikumana walifunga ndoa mwaka 2009 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume, lakini ndoa yao haikudumu muda mrefu na kutengana, hivyo sasa Ndikumana ameonyesha kuridhia kutoa talaka kwa msanii huyo wa bongo movie.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364