-->

Hivi Ndiyo Vitu 3 Vilivyomvutia Wolper kwa Harmonize

Jacqueline Wolper amevitaja vitu vitatu ambavyo vimemvutia kuwa kwenye mahusiano na Harmonize.

Muigizaji huyo amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM, vitu hivyo ni upole wake, ukarimu pamoja na kuijua dini.

“Upole, Ukarimu na anapenda dini na anaijua dini kabisa. Mimi naamini asingekuwa mwanamuziki angekuwa maalimu fulani hivi,” amesema Wolper.

Wakati huo huo Harmonize kwa sasa ameachia wimbo mpya ‘Niambie’ ambao amemuimbia mpenzi wake Wolper.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364