-->

Upelelezi Kesi ya Wema Mbioni Kukamilika, Yapigwa Kalenda

Dar es Salaam. Upelelezi wa kesi ya kukutwa na bangi inayomkabili Msanii maarufu nchini wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu (28) na wenzake wawili akiwemo mfanyakazi wake wa ndani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upo katika hatua za mwisho kukamilika.

Wema Sepetu

Wakili wa Serikali Constantine Kakula ameeleza hayo leo (Jumatano) mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba aliuhimiza upande wa mashtaka wajitahidi kuukamilisha na kesi imeahirishwa hadi Aprili 11 ,2017.

Mbali na Wema wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni mfanyakazi wake wa ndani, Angelina Msigwa (21) na Matrida Seleman Abbas (16) aliyetambuliwa kuwa ni mkulima wote wanatetewa na wakili Hekima Mwesigwa.

Mwananchi

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364