Hivi Punde: Mke Mdogo wa Mzee Yusuf Amefariki Usiku Huu
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Bendi ya Jahazi Modern, Mzee Yusuf amefiwa na mkewe usiku huu. Mmoja wa Wakurugenzi wa Jahaz Modern Taarab, Mzee Juma Mbizo ameiambia Global Publishers kuwa bi Chiku, ambae alikua mke mdogo wa Mzee Yusuf amefariki dunia katika Hospitali ya Amana wakati akijifingua. Mtoto nae pia amefariki.
Pumzika kwa amani Chiku. Pole kwa Mzee Yusuph ndugu jamaa na marafiki.