-->

Huyu Wolper ukimzingua tu, anakumwaga

“Kila mtu anatakiwa kuwa na maamuzi yanayompa faraja, si kila jambo lazima liwe sawa na mtu mwingine kifikra, kuna baadhi ya wanawake wanajikuta wakinyanyasika kwa kuhofia jamii itawaonaje wakiachana na waume wasaliti, ila kwangu haipo hivyo,” alisema.

JACQUELINE Wolper, mmoja wa nyota wa filamu nchini amesema hajaumbwa ili ateseke au kunyanyasika kwa mwanaume, hivyo anapokuwa na rafiki wa kiume na kubaini ni mbabaishaji, lazima ammwage fasta bila kujali jamii itapokeaje jambo hilo au itamlaumu vipi.

“Kila mtu anatakiwa kuwa na maamuzi yanayompa faraja, si kila jambo lazima liwe sawa na mtu mwingine kifikra, kuna baadhi ya wanawake wanajikuta wakinyanyasika kwa kuhofia jamii itawaonaje wakiachana na waume wasaliti, ila kwangu haipo hivyo,” alisema.

Wolper aliongeza kusema kwake ni ujinga kumvumilia mwanaume asiye na mapenzi na mwenye matukio ya kuudhi.

“Kama mtu atakuwa na maamuzi ya mapema, ni vyema kuendelea na maisha yake kwa amani. Utamaduni huo ninao mimi sitaki kuumizwa hovyo,” alisisitiza.

Mwanaspoti

Comments

comments

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364