-->

Idris Aingilia Bifu la Diamond, Dimpoz, Kiba

WAKATI gumzo la mvu­tano na kutupi­ana vijembe kwa wasanii watatu, Diamond Plat­numz, Ommy Dimpoz na Ali Kiba likiendelea, mshindi wa shindano la Big Brother Afrika 2014, Idris Sultan naye ametoa neno kuhusiana na hicho kina­choendelea.

IDRISS231

Wasanii hao wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba‘King Kiba’ na Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz ’ wamekuwa  wakionekana kuwa karibu siku za hivi karibuni na kutupiana vi­jembe na rafiki wao wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond’, hali iliyo­fanya kuwa na mgawanyiko wa mashabiki wanaounga mkono kila upande.

Idris ambaye pia ni mchekeshaji na mtangazaji wa redio, amewa­chambua wasanii hao kitabia na kueleza kile ambacho kinaweza kuwafanya wapatane.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Idris alikuwa na uhusiano wa ki­mapenzi na Wema Sepetu am­baye pia aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond.

“Bifu la Diamond, King Kiba na Ommy Dimpoz ninachokijua ina­tokana na kila mtu kujiona kuwa ni bora zaidi ya mwenzake.

“Hilo ndilo tatizo kubwa ambalo limewafanya washindwe kuele­wana na ndiyo maana wanaibua sinema kila kukicha. Hao wote ni jamaa zangu na ninafahamu vizuri tabia za kila mmoja wao.

TABIA ZA KIBA, DIAMOND, DIMPOZ

“Kiba ni mtu mwenye majigambo, siku zote anaamini kila anach­okiweza yeye hakuna mwingine anayeweza kuwa juu, ikitokea amezidiwa basi ishu ya majigam­bo ndipo inapoanzia na kujikuta akikosana na wenzake.

“Dimpoz ni mtu mvivu sana, yaani huwa hapendi kujibidiisha katika maendeleo yake hadi asu­kumwe, hivyo tabia hii mimi naona kama ndiyo kisa kinachosababi­sha kushindwa kufanikisha mam­bo yake mengi na mwisho wa siku anajikuta akiishia kugombana na wenzake.

“Diamond namuona mchapaka­zi sana na anapenda maendeleo ya haraka kiasi kwamba akiona kama kuna mtu anataka kuremba mbele yake huwa hakawii kumpu­uza huku akiendelea kufanya mambo yake.

“Ila Diamond naye ana vijitabia vya uswahili-uswahili hivi, mfano kupigapiga vijembe, hii inatokana

na mazingira aliy­okulia.

“Kwa maelezo haya naamini un­aweza kuelewa kwa nini watu hao ni vigumu kuwa kitu ki­moja.

DIAMOND VS KIBA

“ Hivi unajua ugomvi wa Diamond na Kiba siku zote nimekuwa si­uelewi , maana kila mmoja ni­kimuuliza kwa upande wake, haku­na aliyewahi kunithibitishia kuwa wana­tatizo zaidi ya kutuhumia na juu ya kushindwa kushirikisha na kwenye moja ya kolabo yao.

DIAMOND VS DIMPOZ

“Watu wanatakiwa watam­bue kuwa hawa wana­juana vizuri, kila mmoja ana udhaifu wake, hakuna anayeweza kuwapatanisha labda wao wenyewe waam­ue kuelewana kivyao. Wala siamini kuwa Wema ana­husika kwenye bifu lao.

“Wapo wanaodai kisa ni ile ishu ya Wema kufanya video na Dimpoz, mimi siafiki hilo, ingekuwa hivyo basi Diamond angekuwa ameshanipiga risasi kabisa kwa kuwa nilikuwa mpenzi wa Wema.

“Tumekuwa tukikutana na tunazungumza freshi tu, mimi na Diamond tuna­heshimiana japo kwa sasa siyo rafiki yangu wa karibu na hata tulipokuwa tukiku­tana tulikuwa poa tu.

“Katika bifu hili la Dia­mond na Dimpoz ukichun­guza kwa makini utagundua limeiva baada ya wote wawi­li kuachia nyimbo, hivyo kwa mwenye upeo ataona tu kuwa wana njia ya kupenye­za muziki wao kwa kutumia vijembe.

“Najua ipo siku Diamond na Dimpoz watakuja kupa­tana, waachwe tu, kwa sasa hata waitwe mashekhe na mapadri na uweke viongozi wa kuu wa nchi, kamwe ha­wawezi kuwaweka sawa.

“Bifu lao litakuja kutu­lia tu siku moja wao wawili watakapoamua, kwani hata tukizidi kupiga makelele sana hakuna hata mmoja anayeweza kusema ukweli.

“Kutokana na hali hiyo hakuna haja ya kupigizana kelele hapa, zaidi wana­chotakiwa kukubali wasanii wenzangu ni kwamba, Dia­mond ni mchapa kazi na hapendi wenzake wasifani­kiwe, hivyo tuendelee kusa­potiana na kuiga uchapakazi huo,” anasema Idris.

Chanzo:GPL

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364