Salama Apata Shavu Kuwa ‘HOST EATV AWARDS 2016
Mtangazaji maarufu wa runinga ambaye ni rafiki na kipenzi cha wengi Salama Jabir ataandika historia sambamba na kampuni EATV LTD baada ya kupata nafasi ya kipekee ya kuwa ‘HOST’ wa tuzo za kwanza za EATV
Sherehe hizo za utoaji wa tuzo ambazo ni kubwa zaidi Afrika Mashariki na zinafanyika kwa mara ya kwanza , zitatolewa Desemba 10, 2016 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam
Baada ya East Africa Television LTD kumtangaza Salama Jabir mwenyewe alionyesha kufurahia na alitumia akaunti yake ya Twiiter kuweka ujumbe maalum wa kuonesha furaha yake