-->

Idris Kukimbiza na ‘Karibu Kiumeni’ Bongo Movie!

MSHINDI wa shindano la Big Brother Idris Sultan ametamba kwa kusema kuwa kipaji chake ni kikubwa sana katika fani nyingi lakini kwa upande wa uigizaji anaamini kuwa yupo vinzuri sana na ameingia rasmi kwa ajili ya kuwapoteza nyota waliopo katika tasnia ya filamu kwani anajiamini na ana uwezo mkubwa katika uigizaji na ameingia rasmi kupitia filamu ya Karibu kiumeni.

idriss23

Idris Sultan mwigizaji

“Kabla ya kuingia katika filamu ya Karibu Kiumeni nilisoma mswada kwa umakini na kujiridhisha kuwa hii ni sinema ambayo inafungua ndoto zangu za kuwa msanii nyota kabisa barani Afrika na Ulaya pia nimeliona hilo kukutana na mwigizaji bora kama Ernest wa Going Bongo si mchezo,”alisema Idris.

idriss032

Ernest akiwa na Idris Sultan katika filamu ya Karibu Kiumeni.

Idrasa ni mmoja kati ya wasanii walioshiriki katika filamu ya Karibu Kiumeni sinema iliyoongozwa na muongozaji mkubwa wa filamu Bongo na wa kimataifa Nick Marwa aliyeongoza sinema kubwa ya Going Bongo katika sinema hiyo iliyojaa nyota wengi Idrasa anasema kuwa amefanya makubwa Bongo na kuwa tishio kwa wasanii wa Bongo Idris amekuwa akitamba katika fani ya uchekeshaji.

 

Director Nick anakubali sana uwezo wa Sultan na kazi ambayo italeta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu Swahilihood ni kazi kubwa kama ilivyokuwa Going Bongo filamu ambayo itwaha tuzo kadhaa ulimwenguni.

Filamu Central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364