Idris Sultan Azungumzia Karibu Kiumeni, Utani Wa Diamond Na Alikiba & Mengine – (Video)
Idris Sultan ni miongoni mwa vipaji vipya vitakavyoonyesha uwezo wao wa kuigiza kwa mara ya kwanza kupitia filamu mpya ya Mtanzania Ernest Napoleon, ‘Karibu Kiumeni’.
Camera za Global TV Online zilikutana na Idris Sultan kwenye press screening ya filamu mpya ya Karibu Kiumeni na kupiga nae stori. Miongoni mwa vitu alivyoviongelea ni pamoja na nafasi aliyoicheza kwenye filamu ya Karibu Kiumeni ya muuza dawa za kulevya:
” Character ilitengenezwa vizuri sana, nimependa sana kitu Ernest alichofanya ni kwamba amekuja kumchagua mtu msiyemtegea kuwa angechaguliwa, ni kitu ambacho kimeshitua watu kwasababu hamuwezi kutegemea kuwa Idris ata-act serious na ku-act character ambayo haijachekesha, ambayo haina comedy yoyote mle ndani zaidi ya kufanya real life. “ Aliongezea:
” Ukiwa commedian una-act masiha tofauti tofauti sana, so naweza kuwa serious hata kama watu hawajui kama naweza kuwa serious na target yangu kubwa ni Hollywoodna kitu ambacho naweka focus kubwa sana… so character kama hizi zinanionyeshajinsi ambavyo naweza fanya vitu tofauti na kufikilsha lengo langu… “
Mbali na utani wake, Idris hakusita kutoa wito kwa ‘serious’ movie directors ambao wangependa kufanya nae kazi:
” Character kama hizi zinasaidia kuonyesha kuwa nini uwezo wa kufanya vitu tofauti tofauti, so kama kuna directors ambao wapo serious sana, wanafikiria kufanya kazi na Idris, anytime wanaweza kunifuata…“
Baada ya hapo ilikuwa ni kuvunja mbavu tuu na hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye hizi dakika 13 hapa chini: