-->

Imenichukua Muda Kujikubali – Ebitoke

Msanii wa vichekesho nchini Ebitoke amefunguka na kusema imemchukua muda mrefu sana yeye kuikubali hali yake kama msanii wa kuchekesha na muonekano wake huo aliyonao sasa anapokuwa anachekesha.

Ebitoke amesema kuwa mwanzo yeye alikuwa ni muigizaji wa filamu ambaye alikuwa anaigiza ‘serious movie’ na hakutegemea kama angekuja kuwa mchekeshaji kwani hakuwahi kujua kama yeye ni mchekeshaji.
“Mimi nilikuwa ni muigizaji wa ‘serious movie’ lakini baadaye muongozaji wetu aliniambia nifanye hicho kitu, nakumbuka alisiyo hiyo meneja alimwambia leo naomba mpaka huyu ‘make up’ ya tofauti mimi nikajua kuwa napakwa kwa kurembwa, mama yangu kilicholetwa nikasema mama yangu hivi huyu ni mimi kweli nilijiangalia kwenye kioo mpaka nikashtuka sikuwa na jinsi ilibidi nicheze tu lakini kiukweli ilinichukua muda sana kuikubali hii hali ya kupakwa mafuta” alisema Ebitoke
Aidha Ebitoke anasema ilibidi aukubali huo uhusika baada ya kuona watu wengi wanapenda na kuvutiwa nao ila yeye mwanzo alikuwa haupendi muonekano huo wa kupakwa mafuta vile lakini anadai kupitia muonekano huo ameweza kupata heshima kupitia sanaa yake hiyo.
EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364