-->

Irene Uwoya Afungukia Mpenzi Wake Kuwa na Mkovu ya Visu

Msanii wa kike wa filamu za bongo ambaye pia aliwahi kuolewa na mcheza mpira kutoka Rwanda, mlimbwende Irene uwoya, amesema mpenzi wake wa sasa ana ngeu nyingi mwilini za kuchanwa visu.

Akipiga stori na Big Chawa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Irene amesema watu kama hao ndio anaowataka yeye kwani inaonyesha uanaume halisi, na sio mwanaume anakuwa laini kama mtoto wa kike.

“Sijasema napenda wanaume wenye sura mbaya nimesema napenda mwanaume mwenye sura ya kiume, mwanaume uwe na ngeu, mimi bwana wangu ana ngeu, kachanwa visu yani”, alisikika Irene Uwoya akimfungukia Big Chawa.

Irene uwoya kwa sasa hajaweka wazi mahusiano yake tangu kuwe na habari za kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Msami, na amesema hataweka tena mahusiano yake wazi kwenye mitandao.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364