-->

Jackline Wolper: Marafiki Wapya Hutuharibia Maisha

MWIGIZAJI wa filamu za Bongo, Jackline Wolper, ameweka wazi kwamba hataki kusikia habari za kuwa na marafiki wapya, kwa madai kwamba ndio wanaoharibu misingi ya maisha yake.

Wolper aliliambia MTANZANIA kwamba, wakati wa kupata marafiki wapya huwa mzuri, lakini baadaye hujikuta katika matatizo yasiyokwisha.

“Sisi mastaa tuna kazi kubwa, kila siku tunakutana na marafiki wapya ambao kati yao wapo wahalifu wanaojificha kupitia majina yetu na linapotokea jambo baya hujikuta ukijumuishwa ukiwa hujui chochote.

“Nawashauri mastaa wenzangu wa fani zote kuwa makini na marafiki kwa kuwa wengi wao hututumia kwa maslahi yao na katika mambo mengi tusiyoyajua,” alisema Wolper.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364