-->

Jay Moe: Wasanii Wanaokula ‘Unga’ ni Washamba

Msanii wa hip hop nchini Tanzania Jay Moe au wengine wanapenda kumuita kwa jina la mzee wa pesa madafu amekutana na camera ya eNewz na amezungumzia kuhusu swala la madawa ya kulevya ambalo limekuwa gumzo katika siku za karibuni.

Jay Moe

Gumzo hilo limekuwa kubwa hasa baada ya picha za aliyekuwa mshiriki wa Big Brother Africa kuonekana naye kuwa ni mmoja kati ya wahanga wa matumizi hayo.

Jay Moe alisema kuwa kwa upande wake anawaona wasanii wanaokula unga ni wajinga kwa kuwa kama ni stress za muziki watu kama yeye ndiyo wangetakiwa kuwa nazo lakini anaona ni washamba pia akaongezea kwa kusema kuwa wazazi kwa sasa wamekuwa na wasiwasi hata na watoto wao kwa sababu hakuna mzazi anayependa mwanaye kuingia katika madawa ya kulevya

“Mimi nikimuona msanii anatumia madawa ya kulevya namuona mjinga na mshamba, hata kama ni stress za mapenzi haitakiwi iwe hivyo, watu kama sisi kina Jay Moe ambao tulianza muziki kitambo mtu unatoa ngoma kali lakini watu wanakwambia kuwa huna zali ila bado unakaza tu. Inasikitisha inauma na inatutengenezea sisi wasanii picha mbaya sana wazazi wanaona na picha zinasambaa Tanzania nzima na sasa kila mzazi amekuwa makini hataki mtoto atumie hizo dawa na siyo kitu kizuri kabisa”

Jay Moe ni moja kati ya msanii ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu lakini ngoma yake ya pesa madafu ilimrudisha vizuri sana kwenye game ya muziki.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364